Tanzania Shilling vs United States Dollar (TZSUSD) Chart on Tradingview.com

Ijue Tradingview - Sehemu ya Kwanza

By Kebwesi | Trader Uswahilini | 9 Apr 2021


Kama upo serious kutaka kuingia kwenye biashara hii ya kuuza na kununua sarafu za kimtandao, lazima uwe na zana tofauti tofauti. Zana mojawapo muhimu sana ni tradingview.

Tradingview inakupa chati aina nyingi sana, kutokana na data za masoko tofauti tofauti zikiwemo za madini, shares na hata sarafu aina zote, mfano chati ya TZSUSD. Ili tuweze kuendelea na somo, naomba tumia hii link ya tradingview, ambapo itafungua ukurasa wa kujiunga. Kwenye huo ukurasa, bonyeza kitufe cha 'Start now' kwenye kipengele cha "basic" (Tizama picha hapo chini), ambapo utapata fursa ya kuutumia mtandao huo bila gharama yoyote hadi uje kuwe mzoefu.

Chagua Start Now kwenye Basic ya Tradingview.

Baada ya kubonyeza "Start now", ukurasa wa kujisajili utafunguka ambapo itakuwa ni hiari yako kuchagua mfumo rahisi wa kujiunga na tradingview. Aidha unaweza ukajiunga kupitia usajili wako wa facebook, au google (kama una barua pepe ya gmail), ila kwa ushauri tu, inakuwa vizuri zaidi kujiunga kwa kutumia kitufe cha "Email"

Chagua kujiunga kwa kutumia email kwenye Tradingview

Baada ya hapo utaingiwa kwenye ukurasa ambao utahitaji kuingiza data zifuatazo:

1. Jina unalotaka liwe linasomwa na umma mfano "Kwaku", au "Sharma".

2. Email yako halali ambayo utaitumia kuwasiliana na wasimamizi wa tradingview, na ambayo itatumiwa kuhakiki usajili wako.

3. Nomino (Neno/Maneno siri) utakayo itumia kulinda usajili wako.

4. Bonyeza hapo kukiri kuwa unakubali kutumia mtandao wa tradingview kwa masharti husika.

5. Hapo utapata mtihani mdogo wa kuchagua picha zinazo fanana na jina ulilopewa kama ilivyo kwenye picha ya kulia.

6. Ukimaliza kila kitu kimekaa sawa, basi utabonyeza kitufe hicho cha "create account", na hapo utakuwa umejisajili.

Kurasa la kuingiza data tradingview  Mtihani

Trading view ni zana muhimu sana kwa kuzisoma soko zote za kimataifa, haswa kama unataka kuwa na utaalam wa kiufundi zaidi.

Tumefika tamati ya sehemu ya kwanza la hili somo kuhusu tradingview. Nenda kajiunge ili kesho tutaingia ndani yake na kuzichambua siri zake zote ili uweze kupata ujuzi kwa haraka.

Zaid ya hapo, ili uweze kupata masomo zaidi, bonyeza hapa  kujaza fomu fupi uingie kwenye orodha ya wanao jua siri zote za biashara ya kuuza na kununua sarafu mtandaoni.

Karibuni Nyote.

How do you rate this article?

0


Kebwesi
Kebwesi

Recalcitrant Renegade


Trader Uswahilini
Trader Uswahilini

Karibu ujifundishe kuzisoma soko za hisa au sarafu za mtandaoni kwa kutumia uchambuzi wa kiufundi. Uchambuzi kwa kuzisoma chati za masoko kiufundi utakusaidia kuelewa bei za sarafu zinaelekea wapi ukizingatia uchambuzi chanya kupitia vyombo vya habari na matukio mengine. Masomo haya ni kwa wale ambao ni wageni kwenye hii biashara. Tutajitahidi kuwapa siri zote zilizopo ili uweze kufanikisha malengo yako kama mtaalam wa kiufundi kwenye kuuza na kununua sarafu aina zote.

Publish0x

Send a $0.01 microtip in crypto to the author, and earn yourself as you read!

20% to author / 80% to me.
We pay the tips from our rewards pool.