Sirwin
Sirwin
Trader Uswahilini.

Chati za sarafu - Utangulizi

By Kebwesi | Trader Uswahilini | 8 Apr 2021


 

Ukiwa mgeni kwenye hii biashara ya kuuza na kununua sarafu mtandaoni, utakutana na michoro kama hii ifuatayo hapa chini ambayo utaikuta kwenye mitandao kama cryptowat.ch au tradingview.com ambamo nitakushauri uweze kufungua akaunti yako mwenyewe kwa kutumia hiyo link ili tuweze kwenda pamoja kwenye haya masomo.

Chati ya Bitcoin   Chati inayotumia mishumaa (Candlesticks)

Ya kushoto hapo juu inaitwa "Line chart", inafuata mkondo wa bei kwa kutumia huo msitari wa bluu, ilhali hiyo chati ya kulia inaitwa "Candlestick chart", ambapo inakupa picha la soko kwa kutumia mishumaa ya kijani au nyekundu.

Zaidi ya miaka 100 iliyopita, kuna mzee mjapani aliyejulikana kama Homma abaye alivumbua mfumo wa kuzisoma soko ili kuelewa hisia kuu za kipindi husika. Mfano, siku yoyote ile sokoni utakuta labda mpunga umeingia sokoni asubuhi kwa Shilingi 1000 kwa kilo jumla, presha zikapanda na bei nayo ikapanda hadi Shilingi 1400. baadaye wauzaji  wakaongezeka na bei ikashuka hadi Shilingi 600, na baadaye kabisa jioni ukakuta mpunga umepungua ikapanda tena hadi Shilingi 800. Ina maana kwamba bei ya kufungua soko ilikuwa Sh 1000, bei ya kufunga soko ikawa Sh 800, ila bei ya chini kabisa ikawa Sh 600 na ya juu kabisa kwa siku hiyo ikawa Sh 1400.

Mzee huyu wa kijapani aliweza kuchora muhtasari rahisi sana kwa mfanya biashara kusoma na kuelewa soko kwa haraka. Mfano:

Bei ya Soko la mpunga kwa siku moja

Kwa kutafsiri mshumaa huu, tunagundua kuwa hisia ya siku hii ya uuzaji wa mpunga ilikuwa zaidi ni ya kuuza. Yaani mwisho wa siku hiyo wauzaji walikuwa wengi zaidi ya wanunuzi na kwa hivyo waliweza kuiangusha bei na ikafunga siku ikiwa chini ya bei iliyo fungua soko siku hiyo. Kama soko lingefuga bei kubwa zaidi ya iliyofungua, labda Shilingi 1200, basi mshumaa usingekuwa mwekudu, bali wa kijani, mfano:

Soko likiwa limefunga juu ya lilivyo fungua.

 

Hadi hapo tumefika mwisho wa masomo yetu kwa leo. Tutaendelea na somo letu wiki ijayo siku kama hii.

Ili uweze kupata masomo zaidi, bonyeza hapa ili uweze kujaza fomu fupi ili uweze kupata siri zote za biashara ya kuuza na kununua sarafu mtandaoni.

Karibuni Nyote.

How do you rate this article?

0


Kebwesi
Kebwesi

Recalcitrant Renegade


Trader Uswahilini
Trader Uswahilini

Karibu ujifundishe kuzisoma soko za hisa au sarafu za mtandaoni kwa kutumia uchambuzi wa kiufundi. Uchambuzi kwa kuzisoma chati za masoko kiufundi utakusaidia kuelewa bei za sarafu zinaelekea wapi ukizingatia uchambuzi chanya kupitia vyombo vya habari na matukio mengine. Masomo haya ni kwa wale ambao ni wageni kwenye hii biashara. Tutajitahidi kuwapa siri zote zilizopo ili uweze kufanikisha malengo yako kama mtaalam wa kiufundi kwenye kuuza na kununua sarafu aina zote.

Send a $0.01 microtip in crypto to the author, and earn yourself as you read!

20% to author / 80% to me.
We pay the tips from our rewards pool.